Chanzo ajali iliyoua 17 Tanga chatajwa
Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi nchini Awadh Haji, amesema chanzo cha ajali iliyotokea wilayani Korogwe na kuua watu 17 umetokana na uzembe wa dereva wa Fuso aliyekuwa akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake na hatimaye kugongana uso kwa uso na Coaster.

