Hivi ndivyo mnunua madini alivyotoa roho ya mtu
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia Ezekia Luhweshe (31) mchimbaji na mnunuzi wa madini, wilayani Chunya, mkoani Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya wakala wa maegesho ya magari aitwaye William Mgaya (58) mkazi wa Mama John jijini Mbeya.