Jambazi aliyehukumiwa miaka 30 jela akamatwa
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kumkamata Johnson Omary Mchome (39) anayedaiwa kufanya vitendo mbalimbali vya uhalifu (ujambazi) kwa kutumia jina jingine, huku rekodi zikionesha aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa ya unyanganyi.