Iringa yajidhatiti kuwapelekea wakulima mbolea
Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego, amesema yeye pamoja na viongozi wenzake watahakikisha wanakusanya malori yote ya Iringa kwa ajili ya kusambaza mbolea ya ruzuku kwa wakulima ili wasiwe chanzo cha kukwamisha juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan.