Madiwani waaswa kuhusu wavuvi haramu
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba mkoani Kagera hasa wanaowakilisha Kata za visiwani na zile zilizoko katika mwambao wa Ziwa Victoria, wameaswa kutumia nyadhifa zao kuwataka wananchi wanaowaongoza kuacha vitendo vya uvuvi haramu maana vinaathiri uchumi wa wilaya na mkoa.