Denmark kuendelea kushirikiana na Tanzania
Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mette Norgaard Dissing-Spandet, amesema nchi yake itaendelea kushirikiana na serikali sambamba na mashirika ya kijamii katika utoaji wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana na stadi za maisha ambazo zitawasaidia kujiendeleza kiuchumi kwa kujiajiri.