Madereva walevi wafungiwa leseni Arusha
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, katika kuhakikisha linakomesha matukio ya ajali kuelekea mwisho wa mwaka limeendelea kutoa elimu kwa madereva na kuwafungia leseni za udereva madereva watano (05) kwa makosa mbalimbali ikiwemo ulevi na mwendokasi.