Wafanyakazi walalamikia ujira mdogo
Katika kuelekea sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, baadhi ya wafanyakazi kutoka katika sekta mbalimbali zilizo za serikali na zisizo za serikali nchini Tanzania wamelalamikia mishahara midogo isiyoendana na ukali wa maisha.