"Waajiri lindeni afya za wafanyakazi"Ndalichako
Waajiri nchini wametakiwa kuwa na programu endelevu za mazoezi kwenye maeneo yao ya kazi kwa lengo la kuwalinda wafanyakazi dhidi magonjwa yasiyoambukiza ambayo kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni yamekuwa chanzo kikubwa cha vifo.