Wahudumu wapiga pesa za wagonjwa feki wa VVU
TAKUKURU mkoa wa Tanga imewabaini watumishi wa afya katika wilaya ya Muheza waliohusika kusajili wagonjwa hewa 313 wa virusi vya Ukimwi (VVU) ili kuonyesha takwimu zipo juu za wanaoishi na VVU kwa maslahi yao binafsi ikiwemo kujinufaisha na fedha zinazotolewa na shirika la afya la AMREF.