Bilioni 46.89 kulipa walioondolewa kazini
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameridhia kuwa watumishi wote walioondolewa kazini kwa kughushi vyeti warejeshewe michango yao tu waliyokatwa kwenye mishahara na kuwasilishwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kuidhinisha shilingi Bilioni 46.89 zilipwe kundi hilo.