Wakili Mkuu wa serikali ataka haki kwa wawekezaji
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt Boniphace Luhende, amewataka watumishi wa ofisi hiyo kuhakikisha wanatenda haki pale wanaposimamia mashauri ya serikali na wawekezaji wanapokuja kuwekeza hapa nchini ili kurudisha imani waliyonayo kwenye sekta mbalimbali za uchumi hapa nchini.