Kimbunga Roslyn kuipiga Mexico leo.
Miji iliyoko Pwani ya Pasifiki ya Mexico inajiandaa kwa kimbunga kikali kiitwacho Roslyn chenye nguvu, huku kukiwa na tahadhari kwamba kinaweza kuleta ongezeko hatari la dhoruba na mafuriko. Huduma za dharura za ndani zimekuwa zikifanya maandalizi ya dakika za mwisho.