Sekta binafsi yachochea ukuaji wa utalii
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amesema serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi kama kichocheo cha kukuza sekta ya utalii hapa nchini hivyo imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuleta mageuzi hususani katika sheria na maboresho ya sera ya bajeti.