Wafugaji wahatarisha vyanzo vya maji Morogoro
Serikali Wilaya ya Morogoro imesema haitakubaliana na hatua ya wafugaji ambao wanaingiza mifugo yao kwenye vyanzo vya maji ambavyo vinatiririsha maji kwenye mto Ruvu unategemewa na wakazi zaidi ya milioni saba wa mikoa ya Morogoro, Pwani pamoja na Dar es Salaam.