Bil. 3.8 kujenga madarasa mapya Rukwa-Rc Sendiga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga amesema atahakikisha fedha zote zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mapya 191 kwenye shule za sekondari mkoani humo zinatumika kama ilivyokusudiwa ili wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023 waweze kuanza masomo yao kwa wakati.