Bodaboda waliopora wanusurika kuchomwa moto
Vijana wawili waliokuwa na bodaboda wamenusurika kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali, maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, hii leo Julai 7, 2022, baada ya kupora pochi ya mwanamke na kukimbia na baadaye walizingirwa na kuanguka chini.