Region: 
Dar es salaam
District: 
Kinondoni
Donation: 
Taulo za kike kwa wanafunzi 59 kwa mwaka mzima

Kampeni ya Namthamini ya East Africa Television na East Africa Radio ilifika katika shule ya sekondari Turiani iliyopo Magomeni Turiani katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika Duniani inayofanyika Juni 16 kila mwaka.

Lengo la kampeni hii kufika katika shule hiyo ni kutoa elimu ya hedhi sambamba na kugawa na taulo za kike kwa wanafunzi wa kike wanaotoka katika mazingira magumu.

 

wanafunzi wa kike 59 wa shule ya Turiani wamekabidhiwa taulo za kike kwa mwaka mzima.

Mtangazaji wa East Africa TV, Najma Paul akifurahi na wanafunzi wa Turiani.

Wawakilishi wa Rotary Club of Dar es Salaam ambao ni moja ya wadhamini wa kampeni ya Namthamini katika picha ya pamoja na wanafunzi

Wanafunzi wa kiume nao walipata nafasi ya kuzungumza katika kampeni ya Namthamini

Hii ni shule ya tano iliyofikiwa na Kampeni ya Namthamini ndani ya msimu wa 6