Bei ya samaki yapaa

Jumatatu , 20th Jul , 2020

Wafanyabiashara na wachuuzi wa samaki jijini Dar es Salaam wamesema kwa Sasa samaki wamepanda Bei kwa ndoo ndogo kutoka 15000 Hadi Elfu 50000 na elfu 30000 Hadi 90000 kwa ndoo kubwa.

Moja ya wachuuzi wa samaki Dar es Salaam

Wafanyabiashara na wachuuzi wa samaki jijini Dar es Salaam wamesema kwa Sasa samaki wamepanda Bei kwa ndoo ndogo kutoka 15000 HadiĀ  Elfu 50000 na elfu 30000 Hadi 90000 kwa ndoo kubwa.

Hii leo Eatv saa Moja imetembelea masoko kadhaa na kuzungumza na wamiliki wa vyombo vya Majini,wavuvi pamoja na wauzaji wa samaki ambao wameelezea jinsi Hali ilivyo kwa sasa.

Kwa upande wao kinamama ambao hufanya biashara hiyo jijini hapa wamesema changamoto ni kubwa mtaani ambako wateja Wanapata tabu kumudu Bei ya samaki.

Ni zaidi ya wiki moja Sasa Tangu Mamlaka ya Hali ya hewa itoe taarifa juu ya uwepo wa upepo Mkali kwa mikoa ya Lindi Mtwara na Dar es Salaam Hali inayopelekea changamoto kwa wavuvi baharini.