DSTV yaja na ofa mpya

Jumanne , 3rd Mar , 2020

Kampuni ya Multi Choice Tanzania DSTV, wamezindua kampeni yao mpya ya Jiongeze Tukuongezee, ambapo watajea wake wataweza kulipia kifurushi  cha juu na kuongezewa kinachofuata.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa DSTV Ronald Baraka Shelukindo (kulia) akiwa na Yusuph Mlela wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo.

Akiongea na Waandishi wa Habari katika uzinduzi huo uliofanyika ofisi za DSTV Kinondoni Dar es salaam, Mkuu wa kitengo cha thamani kwa wateja, Hilda Nakajumo amesema,

'Mteja ukiwa na kifurushi cha Bomba ukalipia cha Family unaongezewa mpaka kifurushi cha Compact na ukiwa na Family ukalipia Compact unaongezewa Compact Plus na ukiwa Compact ukalipia Compact Plus unapelekwa kifurushi cha Premium ambapo utaweza kuweza kushuhudia michezo yote duninia na burudani nyingine nyingi zikiwemo tamthilia'.

Mapema leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ambapo yalifanyika matembezi

Naye Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa DSTV Ronald Baraka Shelukindo, amesema huu ni mwendelezo wa ofa zao mbalimbali, huku akiwataka watu kuchangamkia fursa hiyo ndani ya mwezi Machi.

Kwa upande wake Balozi wa DSTV muigizaji Yusuph Mlela amesema ubora wa ofa hiyo unawagusa moja kwa moja mashabiki zake na watanufaika na kuweza kutazama tamthlia aliyoshiriki ya Sarafu ambayo inarushwa kupitia chaneli ya Maisha Magic Bongo.

Tazama Video zaidi hapa chini