Ijumaa , 3rd Aug , 2018

Imeelezwa kuwa vijana wengi hasa wanafunzi wa ngazi mbalimbali za elimu wanaweza kutumia fursa walizonazo katika mazingira yanayowazunguka kupata pesa, na moja ya njia hizo ni kutambua kile walichonacho hasa akili na miili yao katika kuitumia na kuanzisha mtaji .

Pesa za Kitanzania

Mmiliki wa  taasisi  inayojihusisha na kuwasaidia  wanafunzi, inayotambulika  kwa jina la SAVE THE STUDENTS kutoka Uingereza, Owen Burek   aliyoianzisha mwaka 2007 akiwa mwanafunzi wa  chuo kikuu cha Manchester , anasema namna ya mwanafunzi kutengeneza pesa,  ni kutumia mtaji wa kwanza ambao ni kuuza elimu yake anayoipata chuoni au shuleni.

Katika nukuu yake Burek anasema "waweza kupata pesa kwa kuanza kuandika vitabu, kufanya kazi za vibarua, kuanzisha biashara mtandaoni,kutumia kipaji kama kuigiza au kuchekesha,kupangisha chumba au nyumba yako na pia kutafuta kazi ya kusambaza huduma hasa chakula”.

Aidha taasisi hiyo ya 'SAVE THE STUDENTS' inaeleza kuwa mwanafunzi anaweza kutumia mwili wake kama mtaji kwa kujiunga na kampuni za mitindo au kufanya kazi za kutumia nguvu ila siyo kutumia mwili kwa matokeo hasi, pia kuanzisha kurasa za kuzungumzia mijadala ya mahusiano au hoja yoyote katika mtandao ambayo inaweza kugusa hisia za watu na kutumia kuzalisha kipato.

Kwa upande wake bilionea na mmiliki wa kampuni ya uzalishaji wa filamu duniani (ALIBABA) Jack Ma(kutoka China) ambaye ni Mwanafalsafa katika nukuu yake anasema “wenye ujuzi huwatumia wapumbavu kusonga mbele, bila mtandao hakuna Jack Ma, mwanafunzi atakayeitambua teknolojia vizuri ndiyo njia ya kukuza uchumi wake, na usipokata tamaa ndiyo njia ya kushinda”.

Kulingana na ripoti ya Baraza la Vyuo Vikuu Afrika Mashariki (IUCEA) ya mwaka 2014 inaonesha kuwa wanafunzi wanaohitimu elimu ya sekondari na  vyuo vikuu ni 600,000 mpaka 800,000 kwa mwaka , na wanafunzi hao ni sehemu ya asilimia 54 ya wasiopata ajira huku asilimia 61 hawakidhi viwango katika soko la ajira.