Mama la Mama Tumaini Anania akabidhiwa zawadi

Jumapili , 9th Mei , 2021

Kampeni ya Mama la Mama iliyokuwa inaendeshwa na kituo cha East Africa Television,  imefikia kilele leo Mei 9, 2021, kwa kumkabidhi mshindi wa mama bora ambaye ni Tumaini Anania, zawadi zake mbalimbali ikiwemo hundi ya shilingi milioni moja.

Mbali na milioni moja, mshindi huyo pia amekabidhiwa jiko la gesi la Kisasa, King'amuzi cha DSTV pamoja na mlo wa mchana kwenye hoteli ya Levant Masaki jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi zake Mama la Mama huyo Tumaini Anania, amewashukuru wadau walioendesha shindano hilo na kusema kuwa zawadi hizo zitamsaidia kujikwamua kiuchumi ikiwemo kuendeleza biashara alizokuwa anaziendesha yeye na Mwanaye.

Kwa upande wa wadhamini wa kampeni hiyo Benki ya UBA, Jaden Store, Dstv, Lavante na Eatv wamesema lengo la kampeni hiyo ni pamoja na kumsaidia mwanamke kujikwamua kiuchumi lakini pia kujali umuhimu wa Mama duniani ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya Mama Duniani.