Jumatano , 18th Mar , 2026

Nyota wa Senegal, Sadio Mane, ametoa tamko kali akilalamikia hali ya soka barani Afrika kufuatia matukio ya hivi karibuni yaliyozua utata hasa Kufutwa kwa Ubingwa wa Afcon kwa Senegal na Kumpatia Morocco

Senegal wakishangilia ubingwa wa AFCON

“Kilichotokea kimezidi mipaka. Huu si mpira tunaoupigania, wala si Afrika tunayoamini. Kuna rushwa nyingi sana katika mchezo wetu, na inaua hamasa ya mamilioni ya mashabiki barani. Wachezaji wanatoa kila kitu uwanjani, lakini maamuzi yanayofanyika nje ya uwanja ndiyo yanaamua matokeo ya mechi na mataji.” - Mane

Ameongeza kuwa amevunjika moyo si kwa ajili ya Senegal pekee, bali kwa soka la Afrika kwa ujumla. Mané amesisitiza kuwa hali hiyo inaathiri taswira ya mchezo huo na kupunguza imani ya mashabiki katika ushindani wa haki.

“Nimevunjika moyo sana, si kwa ajili ya Senegal pekee, bali kwa soka la Afrika kwa ujumla. Tunastahili yaliyo bora zaidi. Mashabiki wanastahili haki, uwazi na heshima,” - Mane