Jumatatu , 17th Mei , 2021

Serikali imetoa siku 14 kwa Kampuni zote ambazo zimesimama Uwekezaji ama zilikwazwa kwa namna yeyote ile kuandika barua barua Wizara ya Uwekezaji Ili kutanzua mikwamo hiyo.

Waziri wa Uwekezaji Geoffrey Mwambe.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Uwekezaji Geoffrey Mwambe wakati akizungumza na wanahabari pamoja na watumishi wa Kituo Cha Uwekezaji nchini Tanzania (TIC)

"Kuna tabia ambayo haziko sawa kwa wenzetu wa sekta binafsi udanganyifu ni mkubwa na kwa sasa hatuwezi kuona serikali ikipoteza kodi stahiki hivyo niwaombe tushirikiane kwa pamoja kuchagiza sekta hii kuzidi kukua"amesisiza Mwambe.

Sambamba na hilo pia ametoa onyo kwa wafanyabiashara na wawekezaji ambao ni wamekuwa wakifanya udanganyifu hasa katika malipo ya ongezeko la thamani (VAT) kubadili tabia kwa kuwa serikali haiko tayari kuona vitendo hivyo vikiendelea.

"Tunataka sasa Uwekezaji nchini ufanyike kupitia Kituo Cha Uwekezaji lakni pia Wizara ya Uwekezaji kwa ujumla hii itapunguza mlolongo" amesema Mwambe.

Katika hatua nyingine amesema kuwa kwa sasa wanashughulikia kubadilisha  madhaifu yalipo kwenye Sheria ya Uwekezaji ya sasa ili masuala yote ya kiuwekezaji yaweze kuratibiwa chini ya Wizara ya Uwekezaji na Taasisi zake Ili kuondoa urasimu.

Baadhi ya mambo ambayo yametajwa kuharibu Uwekezaji ni Vitendo vya Rushwa,udanganyifu kutoka kwa wawekezaji,pamoja na ukwepaji wa kodi sahihi za serikali.