Tigo yatenga Milioni 500 kwa wateja wake

Jumatatu , 25th Nov , 2019

Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini ya Tigo, imezindua promosheni kabambe itakayowawezesha wateja wake kuingia kwenye nafasi ya droo na kujishindia fedha taslimu kila wafanyapo malipo kwa njia ya Tigo Pesa.

Meneja wateja maalumu wa Tigo pesa Mary Ruta (kushoto).

Akizindua promosheni hiyo leo Novemba 25, 2019, Meneja wa wateja maalumu wa Tigo Pesa Mary Ruta, amesema kuwa promosheni hiyo pia imezingatia vigezo na masharti vinavyomtaka mteja lazima awe na kiwango cha shilingi 10000 kwenye akaunti yake.

"Promosheni hii imelenga wateja wa Tigo Pesa zaidi ya 30 kila mwezi na kila wiki watapatikana washindi wa jumla" amesema Ruta.

Promosheni hiyo ni maalumu zaidi katika kuelekea katika msimu wa sikukuu ya za Christmas na Mwaka Mpya.