Jean-Jacques Ndala
Kamati hiyo imemtaja Ndala kama shujaa wa waamuzi ambaye hakutetereshwa na changamoto yoyote alipokuwa akichunguza mechi, na kuonyesha ukomavu, utulivu, nidhamu na maadili katika kila mechi aliyochezesha.
Ndala anakumbukwa kwa kuamua mechi ya ufunguzi ya AFCON 2025 kati ya Morocco na Comoro, na pia alipewa jukumu la kuchezesha fainali kati ya Morocco na Senegal, ambayo ilishuhudia dosari dakika za mwisho kutokana na utata wa mkwaju wa penalti.
Kamati imesema kuwa kupitia utendaji wake, Ndala ameiheshimisha DR Congo na kuenzi heshima ya waamuzi wake barani Afrika, akionyesha mfano wa kitaaluma kwa waamuzi wengine.






