Jumapili , 2nd Oct , 2022

Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), imewapongeza walipakodi wote kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari na kuiwezesha mamlaka hiyo kufikia kiwango cha juu cha makusanyo kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata

Pongezi hizo zimetolewa na Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata, baada ya mamlaka hiyo katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2022/2023 yaani kuanzia Julai hadi Septemba mwaka huu, kukusanya shilingi trilioni 5.923 sawa na ufanisi wa 99.1% ya lengo la kukusanya trilioni 5.978

"Ufanisi huu wa kiuendaji ni matokeo ya kuendelea kuimarika kwa matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika usimamizi wa kodi, kuboreka kwa mazingira ya ufanyaji wa biashara nchini kuimarika kwa ulipaji kodi kwa hiari," imeeleza sehemu ya taarifa ya Kamishna wa TRA