
Katika taarifa ya waandishi wa habari iliyotolewa leo Jumatatu, Juni 9, NPS imethibitisha kusimamishwa kwa Afisa Mkuu wa Kituo cha Polisi, OCS, afisa aliyekuwa kazini usiku huo, afisa anayesimamia seli, na maafisa wote ambao walikuwa kazini usiku huo.
Inspekta Mkuu wa Polisi, Douglas Kanja, ameagiza kuchukuliwa kwa hatua hiyo kuruhusu uchunguzi ufanyike kwa ukamilifu, usio na upendeleo, na wa haraka juu ya suala hilo ambao unaongozwa na chombo huru cha kusimamia polisi nchini Kenya (IPOA).
IPOA imeanzisha uchunguzi kuhusu kifo Ojwang ambaye alikuwa amezuiliwa "kwa uchapishaji wa taarifa za uongo.
Babake Ojwang, Meshack Opiyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa mwanaye alikamatwa kutokana na chapisho kwenye mtandao wa X katika mji wa magharibi wa Homa Bay na kisha kusafirishwa kilomita 350 hadi mji mkuu, Nairobi.