Jumatatu , 3rd Oct , 2022

Wakati ulimwengu mzima ukiadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, kampuni ya Vodacom Tanzania imesema ili kuhakikisha kwamba wateja wake wote wanapata huduma stahiki imeamua kuzindua dawati maalum la huduma kwa wateja wenye mahitaji maalum ili kuweka usawa wa utoaji huduma.

Harriet Lwakatare, Mkurugenzi huduma kwa wateja Vodacom Tanzania

Harriet Lwakatare ambaye ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania, amesema Kila mwaka huwa wanasherekea wiki ya huduma kwa wateja, lakini kwa mwaka huu wanafanya hivyo chini ya kaulimbiu ya ‘tunasherekea kukuhudumia’ .

Kwa upande wake mmoja kati ya wateja wa Vodacom ambaye ni mlemavu wa miguu, Bw. Ernest Justin ameeleza namna dawati hilo maalum lilivyo mhimu kwao, na kwamba kama mtu mwenye ulemavu amefurahi sana kuona wamepewa kipaumbele na Vodacom, huku akisema kuwa walichokifanya ni zaidi ya upendo na kuyaomba makampuni mwengine nchini kuiga kilichofanywa na Vodacom. 

“kwakweli sisi hasa mimi mwenyewe kama mtu mwenye ulemavu nimefurahi sana kuona tumepewa kipaumbele na Vodacom, hiki walichokifanya ni zaidi ya upendo kwetu kwamba sasa kama mtu ni kipofu au kiziwa atahudumiwa na watu wajuzi wa lugha za alama. Na pia niyaombe makampuni mwengine nchini kuiga kilichofanywa na Vodacom. Wametuthamini sana kwa kuanzisha dawati la watu wenye mahitaji maalum" - Ernest Justin  - Mteja wa Vodacom.