Ijumaa , 31st Jul , 2020

Umoja wa vijana Wafanyabiashara wa Mchanga na kokoto katika eneo la ubungo External Jijini Dar es Salaam, umeiomba Serikali kupitia vitengo vya ujenzi vya ngazi ya Halimashauri kuwapa tenda za kutoa huduma ya mchanga na kokoto ili kusaidia kuwakuza kiuchumi.

Ikiwa hii leo ni Sikukuu ya Eid el Haji Eatv imefika katika eneo hilo na kujionea vijana hao wakiendelea na harakati zao ambapo wamesema wanatamani kupata tenda katika serikali yao kwa kuwa imejielekeza katika ujenzi wa maeneo mbalimbali na wao wanauza vifaa vya ujenzi

Wafanyabiashara hao wamesema kupitia Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini TARURA wanaweza kufanya chochote endapo watapata fursa hiyo ya kutoa huduma ya kuwauzia kokoto.

Kwa upande wake Verani Vicent ambaye amekuwa akisafirisha kokoto hizo amesema biashara hiyo hulipiwa vibali na kodi mbalimbali, huku akishukuru serikali kwa kuendelea kutumia eneo hilo lililopo pembezoni mwa barabara ya Mandela kuweka biashara zao.