
pichani: Bandari ya Dar es salaam
Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo, Desemba 27, 2020, katika kikao chake na Waziri na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania na Menejimenti ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kilichofanyika katika ofisi za TPA jijini Dar es Salaam ambapo amesema taasisi hiyo imebeba taswira ya uchumi wa Taifa.
Majaliwa ameitaka Bodi ya Bandari Tanzania, ihakikishe kwamba mamlaka hiyo inafanya kazi kwa weledi na isisite kuchukua hatua kwa mtumishi atakayebainika kutenda makosa na isimbebe kwa namna yoyote.
Aidha Majaliwa ameweka wazi kuwa miongoni mwa mambo yasiyoridhisha yanayofanywa na mamlaka hiyo ambayo yanaikosesha Serikali mapato ni pamoja na msamaha wa kodi ya zaidi ya sh. bilioni mbili iliyoutoa kwa kiwanda cha saruji cha Mbeya licha ya kukataliwa na kamati ya misamaha