Jumanne , 12th Jul , 2016

Jumla ya Watuhumiwa 30 wa mauaji ya vikongwe na wenye ulemavu wa ngozi(Albino) nchini,wamekuhumiwa kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji hayo.

Waziri wa Katiba na sheria Dkt. Harrison Mwakyembe

Akizungumza jana wakati wa ziara yake Mkoani Shinyanga, Waziri wa Katiba na sheria Dkt. Harrison Mwakyembe, amesema katika miaka ya hivi karibuni tatizo la mauaji ya watu hao yamepungua na watahakikisha wanayakomesha kabisa.

Dkt. Mwakyembe amesema pia serikali itaendelea ktoa adhabu kali kwa watu watakaobainika kuendelea kuhusika na mauaji ya watu hao ili kukaliza tatizo hilo ambalo limeipaka matope Tanzania kwa kuonyesha sio kisiwa cha amani kwa watu hao.

Katika hatua nyingine Dkt. Mkwayembe amesema serikali itaanza mikakati ya kujenga Mahakama za Mwanzo katika kila kata nchi nzima ili kuondoa masongamano wa kesi Mahakamani ambazo zinaweza kuwamriwa kwa haraka.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack amesema kati ya changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na uchakavu wa Mahakama, Uhaba wa Mahakimu na kuwa na Magereza ndogo ambayo haitoshelezi mahitaji kuhusika ya kuwahifadhi wafungwa.