Jumatano , 7th Jan , 2026

Takribani watu 36 wameuawa katika siku 10 zilizopita za maandamano nchini Iran, linasema kundi la haki za binadamu

Shirika la Habari la Wanaharakati wa Haki za Binadamu (HRANA) lenye makao yake makuu nje ya nchi liliripoti kwamba 34 kati ya wale waliothibitishwa kuuawa ni waandamanaji na wawili ni maafisa wa usalama.

Serikali ya Iran haijachapisha idadi rasmi ya vifo lakini imesema maafisa watatu wa usalama wameuawa. 

HRANA pia imesema zaidi ya waandamanaji 60 wamejeruhiwa na 2,076 wamekamatwa wakati wa machafuko, ambayo yalisababishwa na mgogoro wa kiuchumi na yameenea katika majimbo 27 kati ya 31.

Maandamano haya yalianza tarehe 28 Desemba, wakati wafanyabiashara wa maduka walipoingia mitaani mwa mji mkuu kuelezea hasira zao kutokana na kushuka kwa thamani ya sarafu ya Iran dhidi ya dola ya Marekani katika soko huria.