Ijumaa , 24th Apr , 2020

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, amesema kuwa jumla ya waathirika 37  wa Virusi vya Corona nchini wameruhusiwa kurudi majumbani kwao baada ya kupona kabisa maambukizi hayo na kuwapa tahadhari ya kuendelea kujikinga kwani upo uwezekano mkubwa wa kuambukizwa mara mbili.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy ametoa taarifa hiyo leo Aprili, 24, 2020, na kusema kuwa idadi ya visa hivyo hapa nchini imebaki kuwa pale pale ya visa 284, ambapo kati ya hao 10 walishafariki, na 48 wameshapona na kuruhusiwa na waliosalia wanaendelea kupata matibabu.

"Jumla ya watu waliopata maambukizi nchini ni 284, vifo ni 10 na hivyo tukabakiwa na watu 274 na kati ya hao 11 tulishawatolea taarifa kwamba wamepona na kati ya watu 263 watu 108, hawana ugonjwa wowote, kwahiyo leo hii tumewaruhusu watu 37 wameenda nyumbani tusiwanyanyapae ni ndugu zetu, lakini nitoe angalizo hata kama umepona Corona unaweza ukapata tena maambukizi, hivyo niwaombe wajilinde na kujikinga" amesema Waziri Ummy.