Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba mkoani Kagera leo tarehe 14 Desemba 2025.
Makamu wa Rais anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mkoa wa Kagera, itakayofanyika kesho tarehe 15 Desemba 2025.


