
Msako huo umefanyika baada ya kuibuka matukio ya kihalifu ambayo ni pamoja na utekaji magari na kupora fedha za madereva na abiria.
Tume ya kudhibiti matukio hayo iliundwa kwa kujumuisha mikoa mitano ya Nyanda za Juu Kusini kwa kujumlisha mkoa wa Njombe,Ruvuma,Iringa ,Songwe na Mbeya ambapo watuhumiwa 69 wa matukio mbalimbali ya uhalifu wamekatwa na kufikisha jumla ya watuhumiwa 87 baada ya msako huo.