Kituo cha mabasi cha Magufuli Dar es Salaam
Wakizungumza na EATV leo Desemba 12, 2022, abiria hao wamesema kuna changamoto ya wananchi wengi hasa wale wanaosafiri kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka kutofikiwa na elimu hiyo jambo linalosababisha kuendelea kukataa tiketi za mkono ambazo hazina bei za nauli elekezi kama zile za kieletroniki
Kwa upande wake Afisa Leseni Mfawidhi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) Eyudi Nziku, amesema serikali ilishapiga marufuku tiketi za mkono na imekuwa ikitoa elimu ya mara kwa mara kwa wananchi na kusisitiza kwamba abiria wote wanaosafiri kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka kuhakikisha wanakata tiketi mtandao Ili kuepuka kuongezewa nauli.
Naye Meneja wa kituo cha mabasi cha Magufuli Isihaka Waziri, ameeleza ni kwa jinsi gani kituo hicho kilivyojipanga kukabiliana na wimbi la idadi kubwa ya abiria wanaosafiri kuelekea kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka, huku akiwasihi abiria kuwa waangalifu na wapiga debe kwa kuwa kila basi lina ofisi zake ndani ya kituo hicho.