Jumamosi , 9th Aug , 2025

Shirikisho la soka barani Afrika CAF leo Ijumaa Agosti 8, 2025 limetoa viwango vya ubora kwa vilabu barani Africa kwa mwaka 2025, ikiwa ni siku moja kabla ya kufanyika kwa droo ya upangaji wa michezo ya hatua ya awali ya klabu bingwa barani Afrika na kombe la shirikisho Afrika. 

Klabu 75 bora Barani Afrika

Kwenye viwango hivyo vilivyotolewa leo na CAF klabu ya Al Ahly ya nchini Misri ndio inashika nafasi ya kwanza ikiwa na alama 78, Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini ni ya pili ina alama 62, nafasi ya tatu ni Esperance ya Tunisia wana alama 57 na mabingwa wa kombe la Shirikisho 2025 RS Berkane wanashika nafasi ya 4 wakiwa na alama 52. Simba SC ya Tanzania inashika nafasi ya tano kwenye orodha hiyo ya ubora wakiwa na alama 48.

Mabingwa watetezi wa klabu bingwa Afrika klabu ya Pyramids inashika nafasi ya sita ikiwa na alama 47, mabingwa wa Tanzania Yanga SC wapo nafasi ya 12 wakiwa na alama 34, timu nyingine ya Tanzania iliyoorodheshwa kwenye viwango vya ubora ni Namungo yenye alama 0.5 wapo nafasi ya 75.