Jumanne , 16th Sep , 2014

Wakazi wa Wilaya ya Wetemkoa wa Kaskazini Pemba wanaotumia usafiri wa majina wapo katika hatari ya kupata ajali za majini kutokana na kutokuwepo kwa usafiri wa uhakika eneo hilo.

Miili pamoja na mizigo ya waliokuwa abiria wa meli ya MV Spice Islander iliyopata ajali na kuzama kwenye mkondoi wa Nungwi mwaka 2011 ikionekana ikielea kwenye maji.

Usafiri huo ni ule unaoliunganisha eneo hilo na maeneo mengine ikiwemo mijiya Tanga na Unguja tatizo linalotajwa kuanza tangu kuzama kwa meli ya MV Spice Island mwezi Septemba 2011.

Hali hiyo imepelekea Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman kuomba msaada kwa wadau kukarabati bandari ya Wete sambamba na kupeleka vyombo vya uhakika vitakaotumika kwenye safari ili kuhakikisha kuwa wakazi hao wanakuwa na usafiri salama

Akielezea hali ya hatari inayowakumba wakazi wa Wete Mkuu wa Bandari ya Wete Hassan Hamdan Ali amesema kuwa matumizi ya vyombo duni na vinavyosafiri kwa muda mrefu baharini vinaendelea kuongezeka huku hatari ikizidi kuwa kubwa na uthibiti wake kuwa ni changamoto