Serikali inaendelea kutekeleza kwa kasi mpango wa Gridi ya Taifa ya Maji kupitia miradi mbalimbali ya ujenzi wa maji inayotekelezwa katika maeneo yote nchini. Miradi hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama kwa uhakika na kwa muda mrefu.
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), amesema mpango huo ni mkakati mahsusi wa Serikali wa kutumia kikamilifu vyanzo vya maji vilivyopo ili kuwanufaisha Watanzania wote, wakiwemo wanaoishi maeneo ya vijijini na mijini kupitia uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Maji ili kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.




