
Sehemu ya Kontena lililodondoka na kusababisha vifo, eneo la Iwambi, jijini Mbeya.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi jijini Mbeya Mussa Taibu amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana, na uchunguzi unaendelea.
“Ajali hii imehusisha Lori na daladala tatu katika Mlima Iwambi mkaoni hapa na kuzipelekea kudumbukia mtoni , ambapo vifo mpaka sasa ni watu ishirini na majeruhi ni arobaini na tano wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Mbeya”, amesema Kamanda.
Moja kati ya daladala iliyokuwa na abiria likiwa korongoni
Kamanda ameongeza kuwa jiografia ya eneo hilo imechangia ajali mara kwa mara katika eneo hilo, na kuwasihi madereva kuwa makini na kupunguza mwendo barabarani.