Ijumaa , 20th Jun , 2025

Mawaziri wa Ulaya wanatarajiwa kukutana leo kuishawishi Iran irudi kwenye meza ya mazungumzo, Mawaziri hao wa Mambo ya nje watakutana na mwenzao wa Iran Abbas Araghchi mjini Geneva, Uswis leo Ijumaa, kwa matumaini ya kupunguza mvutano kati ya Iran na Israel.

Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, na mwanadiplomasia mkuu wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas, wanashiriki katika mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana kati ya Tehran na serikali za magharibi tangu Israel iliposhambulia Iran wiki moja iliyopita.

Hatua hii Inafuatia tangazo la Rais Trump kwamba ataahirisha uamuzi wowote wa kuingilia kijeshi kwa nchi yake huko Iran kwa majuma mawiili.