Panga
Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Ali Hamadi Makame, akizungumza na waaandishi wa habari ofisini kwake amesema mtuhumiwa ambae ni marehemu alifunga mlango wa chumba chao kisha kumuua mkewe na yeye kujinyonga kwa kutumia chandarua alichokifunga juu ya kenchi.
Kamanda Makame amesema kufuatia tukio hilo hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na jeshi la polisi kwa sababu tukio hilo limetokana na mgogoro wa kifamilia na mtuhumiwa wa mauaji hayo naye amekufa kwa kujinyonga.



