Jumanne , 23rd Mei , 2023

Kijana mmoja ambaye jina lake halijafahamika, akikadiriwa kuwa na umri wa miaka 32-35, amefariki, baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya 15, katika jengo la Derm lililopo Makumbusho mkoani Dar es Salaam

Mmoja Shuhuda wa tukio hilo Sabrina amesimulia kuwa mtu huyo amejirusha kama ajali ya mtu kugongwa lakini ni kitu kimedondoka kutoka ghorofani mpaka chini ambapo walikisikia kishindo.

Pia amesema mtu huyo hafanyi kazi katika jengo alilojirusha na wala sio mkazi wa maeneo hayo.

Kwa mujibu wa Mlinzi wa ghorofa alijirusha mwanaume huyo amesema mtu huyo alikuwa anaenda kuswali sala ya Alfajiri ghorofani ambapo baada ya muda mchache alijirusha.

Video kamili ya tukio hilo la mtu kujirusha kutoka ghorofani Makumbusho tayari ipo Youtube ya #EastAfricaRadio usisahau ku-like na subscribe Youtube channel yetu.