Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli
Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 19, 2021, wakati akiongozi familia, viongozi wa dini na wananchi waliojitokeza kuaga mwili wa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, aliyefariki dunia Februari 17, 2021, na ndipo alipoamua kuusoma hadharani ujumbe alioandikiwa na Waziri huyo.
"Tumefikia mahali sasa tunatishana sana, leo nilitumiwa meseji na Waziri wa Fedha Dkt. Mpango, ambaye amelazwa Dodoma, na ninaomba niusome hapa kwa faida ya wale ambao walikuwa wana-Tweet kwamba amekufa na amenitumia leo asubuhi", amesema Rais Dkt. Magufuli
Aidha Dkt. Magufuli, aliendelea kuusoma ujumbe huo, "Ameniambia Mh. Rais asante sana nimepata ujumbe wako kupitia kwa mke wangu, kwa Neema ya Mungu naendelea vizuri, nakula na ninafanya mazoezi ya kifua na kutembea hao wanaonizushia kifo niliwaombea msamaha kwa Yesu wakati wa sala ya jioni jana, Mungu akubariki na akupe Neema na ujasiri zaidi katika kuliongoza Taifa letu katika wimbi hili".