
Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Afya, Dkt Faustine Ndugulile, na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Hayo ameyabainisha leo Mei 17, 2020, kupitia ukurasa wake wa Twitter, na kumkaribisha kwa moyo wa dhati, Naibu Waziri wa Afya mpya Dkt Godwin Mollel, ambaye ameteuliwa siku ya jana.
"Asante Mh Faustine Ndugulile kwa utumishi wako na ushirikiano mkubwa ulionipatia katika kusimamia Sekta ya Afya nchini, kila la heri katika kuwatumikia wana Kigamboni, hongera Dkt Godwin Mollel karibu Wizara ya Afya, naahidi kukupa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao" ameandika Waziri Ummy.