Jumatano , 11th Mar , 2026

Mkurugenzi Wa Uendeshaji Na Biashara wa EFM TV E Bwana Denis Busulwa ( Ssebo ) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospital ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mkurugenzi Wa Uendeshaji Na Biashara wa EFM TV E Bwana Denis Busulwa ( Ssebo ) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospital ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo cha Ssebo zimethibitishwa na Mkurugenzi wa EFM TVE Francis Majizo kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii akeeleza kuwa taratibu zingine zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa.

“Kwa moyo mzito na machozi mengi, nasikitika kutangaza kifo cha rafiki, kaka, aliyekuwa msimamizi wa ndoa yangu, na mfanyakazi mwenzangu aliyeitumikia EFM na TVE kwa nguvu zake zote, ndugu yangu Ssebo.

Ssebo amefariki usiku huu katika hospitali ya taifa Muhimbili.

"Kwa sasa mturuhusu kuaanda taratibu zote zinazohusiana na msiba huu wa Ghafla, ambao kwa kweli siwezi kuuelezea. Taarifa zaidi tutazitoa baadae.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe” alisema Majizo