Ijumaa , 22nd Aug , 2025

Moria maarufu kama Mama Yusta anasakwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma kwa madai ya kumng’ata mdomoni Kanisia Hinju (30) mkazi wa Kihulu na kung’oa kipande cha nyama kisha kutokomea kusikojulikana.

Moria maarufu kama Mama Yusta  anasakwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma kwa madai ya kumng’ata mdomoni Kanisia Hinju (30) mkazi wa Kihulu na kung’oa kipande cha nyama kisha kutokomea kusikojulikana.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi, SACP Marco Chilya amesema tukio hilo lilitokea Agosti 13, 2025 katika kijiji cha Kihulu, Wilaya ya Nyasa baada ya ugomvi uliosababishwa na mtoto wa majeruhi kupigwa na mtuhumiwa.

Aidha, polisi mkoani humo wanawashikilia pia watu 7 waliokutwa na nyara za serikali ikiwemo meno ya tembo 64, kiboko 145 na ngiri 2 zenye thamani ya zaidi ya milioni 314 pamoja na Michael Lusekero (50) mkazi wa Songea kwa kosa la kutengeneza na kuuza pombe bandia aina ya Konyagi, Master Portable Spirit na Smart Gin bila leseni.