Jumatano , 10th Jul , 2019

Mkazi wa Chamazi Omary Chuma, leo Julai 10, 2019 anatarajiwa kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Pwani, kwa kosa la kumtapeli mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo, baada ya kujifanya ofisa wa Serikali.

Jokate Mwegelo

Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu mkurugenzi wa uchunguzi wa  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), nchini Ali Mfulu, ambapo amesema kuwa Chuma alikamatwa na maofisa wa TAKUKURU, baada ya kupokea taarifa kutoka Kisarawe.

Mfuru ameongeza kuwa, walifanikiwa kumkamata ikiwa ni wiki takribani tatu, zikiwa  zimepita tangu wautangazie umma kuhusu, kukamatwa kwa matapali wengine sita walioshirikiana kufanya utapeli.

''Kati ya watuhumiwa hao, wanne walijifanya ni maofisa wa Takukuru wa vyombo vingine vya dola na wawili walitoka katika kampuni ya simu''

Na kwamba uchunguzi huo, umebaini kuwepo kwa mtandao mkubwa, unaohusisha wafanyakazi wa ofisi mbalimbali zikiwemo za Serikali.