Jumatano , 18th Feb , 2015

Star wa muziki Joh Makini amesema kuwa, kuna umuhimu mkubwa wa kutengeneza mfumo wa kuwaandaa vijana kuanzia ngazi ya chini kabisa.

Joh Makini

Amesema hiyo ni kwa ajili ya kuwaweka tayari kwa nafasi za juu kama vile uongozi katika nchi, hatua ambayo itasaidia kuzuia changamoto nyingi ambazo zinaonekana sasa kwa upande huo.

Joh Makini amesema kuwa, anaona kuna umuhimu mkubwa wa kuanza sasa kuwekeza katika mkakati huu, kutoa elimu kwa vijana, kuwajengea uzalendo na saikolojia ya kurithi nafasi hizo ambazo sasa kwa sehemu kubwa zinashikiliwa na wazee.